Thursday, January 1, 2015

POMBE SIO CHAI: MKE WAKIGOGO AANZA MWAKA VIBAYA BAADA YA KUNYWESHWA POMBE NA KUFANYIWA KITU MBAYA

 
Hii ni aibu nzito! Mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Oliver (pichani) ambaye inadaiwa ni mke wa kigogo wa Wizara ya Mali Asili na Utalii mkoani hapa (jina tunalihifadhi), amejikuta akianza mwaka vibaya kwa kufanyiwa kitu mbaya baada ya kuleweshwa. 
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri hivi karibuni baada ya mwanamke huyo kudaiwa kunyweshwa pombe na wanaume ambao idadi yao haikufahamika mara moja kisha kumfanyia vitendo vya kumdhalilisha.
Mtoa habari wetu aliyeshuhudia mchezo mzima, aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, Januari 3, mwaka huu mida ya jioni, mwanamke huyo alionekana akiingia katika baa moja iliyopo mkoani hapa na kuanza ‘kukata maji’.
Ikadaiwa kuwa, baada ya kunywa chupa kadhaa za bia aliamua kuamka na kwenda kucheza muziki ambapo akiwa kwenye ‘dancing floor’, alipata kampani ya wanaume hao ambao ndani ya muda mfupi alizoeana nao.
“Walicheza sana muziki na ilipofika mishale ya saa nne usiku, Oliver akiwa na wanaume hao walipanda sehemu ya juu ya baa hiyo ambako wateja huenda kupumzika.
 
“Kule juu hatukujua kilichokuwa kikiendelea lakini ndani ya saa moja na nusu hivi, wale wanaume wakaanza kushuka mmoja baada ya mwingine na mwishowe akabaki yule mwanamke mwenyewe kule juu.

“Tukawa na wasiwasi na tulipopanda juu tukamkuta Oliver akiwa amezimika kwenye kochi huku akiwa amevuliwa nguo yake ya ndani.

“Hatukujua walichomfanyia lakini kile kitendo cha kumlewesha na kumvua nguo tu ni udhalilishaji wa hali ya juu,” alisema mtoa habari huyo.

Ikaelezwa kuwa, baada ya wasamaria wema kumkuta mwanamke huyo akiwa katika hali hiyo, walimvalisha nguo kisha kumlaza sehemu salama.

“Cha ajabu sasa, ilipofika asubuhi Oliver alizinduka na kujiweka ‘fresh’ kisha bila ya kuongea na mtu yeyote aliondoka na kuelekea kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.

Jitihada za kumpata mume wa mwanamke huyo ziligonga mwamba kufuatia taarifa kuwa alikuwa safarini.

Alipotafutwa Oliver ili kuzungumzia aibu aliyoipata aliishia kujing’atang’ata huku akieleza kuwa, ameshasahau kwani wanaume waliomfanyia mchezo mchafu huo hawezi kuwatambua hata akikutana nao.

Matukio ya wanawake kuleweshwa kisha kufanyiwa ‘kitu mbaya’, yamekuwa yakishamiri katika maeneo mbalimbali hivyo gazeti hili linawatahadharisha wanywaji wa pombe kuwa makini ili kujiepusha na aibu zinazokwepeka.