Thursday, January 1, 2015

YAMOTO BAND YAUANZA MWAKA VIZURI KWA KUANZA NA SHOO ZA UINGEREZA!

Bendi ya vijana wadogo inayokua kwa kasi kubwa Yamoto Band, imeuanza vizuri mwaka mpya kwa kupata show za kimataifa ikiwa ni mwaka mmoja tu toka itambulishwe rasmi.



Meneja wa Yamoto, Said Fella ametoa ratiba ya bendi hiyo kwa mwaka huu (2015) , na miongoni mwa show wanazotarajia kufanya miezi ya mwanzoni ni pamoja na show ya Uingereza.

Kupitia Instagram Fella aliandika: 

“Aya wadau napenda ya kuwafamisha ratiba ya mwaka huu ya moto band leo tar 1 leo daimond kawaalika rwanda tar 4 tupo maisha club kuzindua ngoma interview tar 10 tupo kigoma tar 31 watawasindikiza wakubwa zao mh temba, chege na madee kwenye utambulisho wa ngoma na video walofanya kaburu ukumbi wa escape 1 na tar 14 mwezi wa 2 watakuwepo musoma na tar 21 ndio MUNGU akipenda vijana watakuwa UK inshaallah MUNGU akipenda”.