SOMO! Mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ametoa tahadhari kwa wasanii kutotumia madawa ya kulevya (unga) ndani ya mwaka huu 2015 huku akiwatupia jicho zaidi nyota wanaofanya vizuri kwenye gemu kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Ray C ambaye ni mmoja wa wasanii waliotumia madawa hayo na kumpa mateso makubwa kisha kuamua kuyaacha, amesema anahitaji kuona wasanii hao wakiwa mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya unga na si wao kuwa wa kwanza kutumia kwani vishawishi huwa vinaibuka zaidi pale msanii anapokuwa juu kimuziki.
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
“Madawa ya kulevya yanatakiwa kupigwa vita sana na kila msanii, wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba sitapenda kuwaona wakizama kwenye matumizi hayo mabaya, nahitaji kuwaona wakiwa katika nafasi za juu, wajihadhari maana umaarufu ndiyo unaoibua haya yote,” alisema Ray C.