Sunday, January 25, 2015

TATIZO LA KUTOKWA NA MAJI MACHAFU KAMA MAZIWA WAKATI WA TENDO NA YENYE KUWASHA MWENZI WAKO, TIBA NA USHAURI

Doctor me ninatokwa na uchafu mweupe kama mazima wakati wa kufanya tendo la ndoa na huwa ukimgusa mume wangu anawashwa,tatizo ni nini maana sikuwa hivyo?

Tatizo hilo ni fangasi za ukeni. Fangasi za ukeni hujulikana kama Candida. Na zile zinazosababisha ugonjwa ukeni zinajulikana kama Candida Albicans. 
Fangasi hawa husababisha mwasho mkali sana, uvimbe kwenye kuta za ukeni na pia mtekenyo. Fangasi hawa pia huweza kuambukizwa kwa njia ya kujamiana ingawa wengi hawazihusishi na magonjwa ya kujamiana. Fangasi hawa hutibika kiraisi sana. Kama hunapata fangasi hawa mara kwa mara au wanarudiarudia basi inawezekana kuwa fangasi hao ni wa aina nyingine hivyo Daktari anahitaji kukufanyia uchunguzi zaidi wa kimahabara. Dalili za Fangasi za ukeni ni pamoja na Mwasho ukeni, Kujikuna ukeni, Kutokwa na uchafu ukeni, mara nyingi unakuwa na rangi nyeupe kama maziwa na pia yanaweza kuwa kama mgando. Wakati mwingine uchafu huu unaweza kuwa kama maji. Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, Michubuko na Viupele. Namna ya kutambua tatizo hili: 
Ukienda hospitali Daktari atachukua maelezo yako namna gani tatizo hili limeanza na kama umewahi kuwa na shida kama hiyo hiyo na dawa ulizokwisha tumia na pia kama umewahi kupata magonjwa yoyote ya kujamiana. Kisha atakufanyia uchunguzi kwa kutazama sehemu zako za siri hususan kwenye kuta za uke na pia ndani kuona shingo ya uzazi. Kutokana na Daktari atakayoona anaweza kuamua kuchukua kipimo kwa ajili ya mahabara. Kipimo hiki kinaitwa “Vaginal Culture” Matibabu ya Fangasi za ukeni Matibabu yanategemea kiwango cha maambukizi pamoja na madhara ya ugonjwa a)Maambukizi madogo: Mara nyingi Daktari wako atakupatia dawa za kumeza kwa siku chache, kupaka au kuweka ukeni. Dawa hizi unaweza kutumia siku moja hadi tatu. Dawa zinazotumika ni kama Gynazole (Gynazle), Lotrimin, Monistat na Terazol. Dozi moja ya dawa ya kumeza inaweza kutumika mfano Diflucan Ushauri: Husitumie dawa yoyote bila kuandikiwa na daktari. Ukihisi una tatizo hili ni vema uende kituo chochote cha Afya kilichokaribu nawe ili umwone 
Daktari kwa matibabu na ufuatiliaji pindi tatizo linarudia katika kipindi cha miezi miwili. b) Maambukizi makubwa: Haya huhitaji matibabu makubwa zaidi. Ukiwa na dalili hizi ni vema ukamuone daktari: Mwasho mkari, Umepata maambukizi ya fangasi mara nne kwa mwaka mmoja, Uvimbe, Ngozi ya ndani imekuwa nyekundu, Una ujauzito, Una kisukari, Au unaishi na virusi vya ukimwi, Matibabu hapa yanaweza kuwa kama ifuatavyo: Siku 14 za kupaka dawa (cream, ointment), vidonge vya kumeza au kuweka ukeni Dozi mbili au tatu za Diflucan (Hii haitumiki kwa mwanamke mjamzito) Matumizi ya dawa kwa muda mrefu angalau wiki sita hususan Diflucan ambayo unameza kidonge kimoja kwa wiki kwa wiki sita au dawa ya kupaka ukeni kwa kipindi cha wiki sita Kumtibu mwenzi wako la sivyo tatizo litarudiarudia. Jinsi ya Kuzuia maambukizi ya Fangasi za ukeni. Ni vema kutambua nini kilikusabibishia kupata maambuki haya. Kwa mfano Wanawake wengine husema walipata maambukizi haya baada ya kutumia dawa za antibiotikisi. Ukitambua kitu kilichokusababishia tatizo hili basi unaweza kuzuia isitokee tena. Mambo mengine ya kusaidia kuzuia maambukizi haya ni: Zuia kuvaa nguo zinazobana Zuia kuosha ukeni kwa kutumia kemikali za kike, cream, sabuni zilizowekewa dawa, deodorants na pads Husivae chupi mbichi Vaa chupi za pamba Kula chakula chenye virutubisho vya lactobacillus kama yogurt Fua chupi kwa maji ya moto Ushauri: Unatakiwa kwenda kumwona Daktari katika vituo vya afya wewe pamoja na mwenzi wako ili mpate tiba ya pamoja kwani kwa kutofanya hivyo tatizo litaendelea kuwasumbueni