Friday, January 30, 2015

WANASWA WAKIFANYA MAPENZI KITUO CHA POLISI

Watu hao wakiendelea kufanya mambo yao.

AMA kweli binadamu siyo waoga! Watu wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja, waliamua kujitoa fahamu na kuamua kufanya mapenzi ndani ya gari nje ya Kituo cha Polisi cha Alimaua kilichopo Kata ya Kijitonyama jijini Dar,
Tukio hilo la aina yake lilinaswa saa nane usiku wa Jumatano 
Awali, baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kuangalia mechi ya Kombe la Capital One kati ya Chelsea na Liverpool nchini Uingereza waliwaona wawili hao wakipaki gari eneo hilo la polisi kana kwamba walikuwa na shida muhimu ya kiusalama kama si kisheria. Kituo hicho kilikuwa kimefungwa!
Tofauti na matarajio ya mashuhuda hao, gari hilo aina ya Toyota Mark II (namba za usajili tunazo) lilizimwa taa za ndani na kuachwa ikiunguruma kisha watu hao ambao haikufahamika kama ni wapenzi au ni changudoa na mteja wake walianza kushikana kimahaba.
DEREVA ALALIA USUKANI
mashuhuda walijiongeza na kubaini kwamba wawili hao walikodi gari hilo kwani walipoanza kushikana, dereva aliegemea usukani kwa hali iliyotafsirika kuwa, alikuwa akiwapa nafasi abiria wake wamalize ‘mambo’ yao.
He! Mchezo wAnoga
“Unaweza kusema wawili hao walikuwa ndani ya fensi nyumbani kwao, kwani wanazidi kufanyiana mambo ya chumbani.
Ndani ya dakika chache, mashuhuda walikuwa wamewasili eneo la tukio.
Kitendo bila kuchelewa, zoezi la kuwafotoa picha kwa mbali lilianza na ndipo waliposhituliwa na mwanga wa ‘flash’, hali iliyomfanya dereva wa gari hilo kutaka kuondoa gari.
WATAITIWA, WAKUTWA CHAKARI
Kwa kutumia ujasiri wa hali ya juu mashuhuda anayeishi eneo hilo walilizuia gari lisiondoke na ndipo ilipobainika kuwa, licha ya kunaswa wakiibanjua amri ya sita ya Muumba pia watu hao walikuwa chakari kwa pombe.
WASHINDWA KUJIBU MASWALI
Hata hivyo, kutokana na kuwa tilalila, ilikuwa vigumu kuwahoji kwani kila walipoulizwa kwa nini waliamua ‘kupumzikia’ nje ya kituo hicho cha polisi, waliishia kuinamisha vichwa.
Uchunguzi umebaini kuwa, kitendo cha watu hao kupaki gari eneo la kituo cha polisi na kufanya uzinzi kilitokana na pombe walizokuwa wamekunywa hivyo akili yao iliwatuma kuwa lile lilikuwa eneo salama zaidi kwao.