Nimeikopi mahali Fulani 1. Tengeneza bajeti. Bajeti
yako ni muhimu na ndio itakayokuongoza kwenye
matumizi yako ya fedha. Jua kila mwezi utatumia
kiasi gani na gawa kwenye wiki na hata siku.
Iheshimu bajeti yako. 2. Nunua vitu kwa jumla.
Kama ni vitu vinavyohusiana na matumizi muhimu
ya nyumbani nunua kwa jumla. Hii itakufanya
ununue kwa bei nzuri na pia kuweza kwenda na
bajeti yako. 3. Sitisha huduma ambazo hutumii.
Kama kuna huduma umejiunga nazo ambazo
hutumii sana sitisha. Hii inaweza kuwa malipo ya
kuangalia tv, malipo ya kuhudhuria mazoezi,
malipo ya gharama za simu na kadhalika. 4.
Usinunue vitu hovyo. Ukikutana na mtu anauza
nguo hata kama umeipenda kiasi gani usiinunue
kama hukuwa na ratiba hizo. 5. Epuka sana
mikopo. Kama kitu sio muhimu sana kwao,
usiingie kwenye mkopo ili kukipata, mikopo ni
mzigo ambao unakupotezea fedha nyingi. 6.
Punguza starehe. Punguza kiasi ambacho
unatumia kwenye starehe kama kula kwenye hoteli
kubwa, kwenda kwenye kumbi za starehe na
kadhalika. 7. Nunua vitu vyenye ubora, hata kama
ni ghali. Unaweza kufikiri kununua vitu vya bei
rahisi ni kubana matumizi ila ukawa ndio
unaongeza matumizi zaidi. Nunua kitu chenye
ubora hata kama ni bei ghali, utakaa nacho muda
mrefu zaidi na hivyo kuepuka kupoteza fedha
kwenye kununua mara kwa mara. 8. Nunua vitu
ambavyo unavihitaji kweli na sio unavyotamani.
Kwa mfano nguo, nusu ya nguo zako hujazivaa
mwaka mmoja uliopita. Sasa unanunua nyingine
za nini? Acha kupoteza fedha. 9. Andaa vitu
unavyoweza kuandaa mwenyewe badala ya kufikiria
kununua tu. Pendelea kupika chakula badala ya
kununua chakula kilichopikwa. 10. Acha kutaka
kuonekana. Usifanye mambo kwa sababu kila mtu
anafanya. Usinunue. simu mpya kwa sababu kila
mtu ana simu mpya. Fanya kitu ambacho unakitaka
kweli na sio kwa sababu kila mtu anakifanya.
Tumia mbinu hizi kumi na uanze kupunguza
matumizi yako mwaka huu 2015.