Friday, February 6, 2015

AUNT AWAPATANISHA WEMA, WIFI YAKE

Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefanya kazi ya ziada kuhakikisha shoga yake, Wema Sepetu na mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye ni mke wa Petit Man, Esma Khan wanapatana.
Wema Sepetu na mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye ni mke wa Petit Man, Esma Khan.
Chanzo chetu kilichokaribu na mastaa hao kilieleza kuwa, awali Wema na Esma walikuwa hawaivi lakini juzi Aunt aliwakalisha na kuwataka wamalize tofauti zao ambapo kila mmoja aliona ni heri iwe hivyo.
 “Si unajua Wema na yule wifi yake Esma walikuwa hawaivi tangu Diamond aamue kuachana naye?
Wema Sepetuakiwa na shoga yake Aunt Ezekiel.
Kimsingi walifikia hatua mbaya, huwezi kuamini kama ni wale waliokuwa wanaitana wifi lakini juzi Aunt kafanikiwa kuwapatanisha,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzipata habari hizo, mwandishi wetu aliwatafuta Wema na Esma bila mafanikio lakini Aunt alipatikana na kukiri kufanya kazi hiyo.