Wednesday, February 11, 2015

BAADA YA Q-CHIEF KUSEMA AMEDHULUMIWA MAMILION NA TID, TID ADAI NI TAMAA NDIO ILIYOMUONDOA Q-CHIEF TOP BAND

Hivi karibuni kupitia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Q-Chief alidai kuwa sababu za kujiondoa kwenye bendi ya TID, Top Band ni baada ya muimbaji huyo wa ‘Zeze’ kumdhulumu mamilioni ya shilingi kutoka kwenye album ya bendi hiyo.

Hata hivyo TID akiongea kwenye kipindi hicho hicho, amedai kuwa hiyo si sababu sahihi na kwamba Chilla alikuwa na tamaa. TID amedai kuwa kimsingi fedha hizo zilikuwa zake zaidi kwa kuwa ni yeye ndiye aliyeandika nyimbo za album hiyo, kutoa jina na pia ni yeye ndiye aliyefikia makubaliano na mhindi kuhusu kuiuza album hiyo.

Amedai kuwa baada ya kulipwa fedha hizo walikuwa wamekubaliana kuwa zingetumika kununulia vyombo vya bendi. Pia alidai Q-Chief alilipwa fedha kadhaa ambazo aliishia kuzilia bata na zilipokwisha aliamua kuchukua polisi kumwendea TID kuwa amemdhulumu fedha yake.