Wednesday, February 11, 2015

MAMBO YAANZA KUMNYOOKEA RAY C,KUANZA UJENZI WA MJENGO WAKE MPYA

Mambo yameanza kumnyookea msanii mkongwe wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’ baada kuonyesha picha ya kiwanja chake kipya kwenye mtandao huku akisema kuwa ataanza ujenzi muda si mrefu.

 Msanii huyo aliandika kuwa madawa ya kulevya yalimpa hasara kubwa ikiwemo kuuza nyumba yake ya zamani ambayo ilikuwa imeisha kabisa lakini sasa anamshukuru Mungu anatimiza ndoto yake ya kuanza ujenzi wa nyumba nyingine mpya.

Aliandika hivi kwenye Instagram….Madawa yalinipotezea nyumba yangu ona sasa naanza upyaaaa!ila sio mbaya namshukuru Muumba wangu kwa Kunitoa kuzimu na kunipa nafasi nyingine tena ya kutimiza ndoto yangu ya kujenga my dream home!

iwe ghorofa au kibanda lakini si changu mwenyewe!hapa nafikiria nishushe kitu gani kwenye hii ardhi ya Nyerere!Mungu in mwema kwangu siku zote............