Thursday, February 5, 2015

Benki ya I&M Yazindua Huduma ya kwanza ya mfumo wa kielekroniki ya masaa 24 katika jengo la Viva Tower, Posta-Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha  (kushoto) akiongea na wadau wa benki hiyo hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa tawi  na mfumo mpya wa kielektroniki uliovumbuliwa na Smart Banking Solutions Ltd ambapo mteja anaweza kuweka na kutoa pesa  sambamba na kupata huduma nyingine za kibenki kama kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mashine za kielektroniki masaa 24 ya siku.Hafla hiyo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja wa I&M wa tawi hilo Bi. Shabina Manji.
Baadhi ya wadau wa benki ya I&M na waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw. Anurag Doreha , hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la kielektroniki , ambapo wateja wake wataweza kuweka na kutoa pesa kwa kutumia ATMs sambamba na huduma ya kubadili fedha za kigeni kwa masaa 24. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi jipya la I&M, Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam. Benki hiyo imeungana na kampuni ya Smart Banking Solutions kuwaletea wateja wake huduma hii
Mkurugenzi Mkuu wa VIVA Tower Viral Manek, akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya I&M katika jengo hilo litakalotoa huduma masaa 24, kwa kuweka na kutoa fedha na kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mfumo mpya wa mashine za kieletroniki (ATMs). Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, Bw. Anurag Doreha, Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha (katikati) akifafanua jambo baada ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo kufanyika katika jengo la Viva Tower ambapo huduma za kuweka, kutoa na kubadilisha fedha za kigeni zitakua zikifanyika masaa 24 kutumia mashine za kielektroniki(ATMs) kulia ni Mkurugenzi mkuu wa VIVA Tower Viral Manek na kushoto ni Meneja Masoko wa Smart Banking Solutions Limited, Salil Abbas Sadik. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam.