Tuesday, February 3, 2015

DK. CHENI KUGOMBEA TENA BONGO MOVIE

MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amefunguka kuwa anasubiri kwa hamu usajili wa fomu ukamilike ili aweze kugombea tena uongozi wa Klabu ya Bongo Movie.
Msanii mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.
Akipiga stori na Uwazi, Dk. Cheni aliweka wazi kuwa ameanza kuona ndoto zake za kuiongoza klabu hiyo zitatimia kwa asilimia fulani kama ambavyo alikuwa akitamani kuwa kiongozi kwa muda mrefu.
“Niko tayari na nitagombea tena uongozi kwa nafasi ya uenyekiti, sasa hivi ninachosubiri ni usajili tu ukikamilika na mambo yatakwenda sawa kwani nimejipanga vya kutosha kuongoza,” alisema Dk. Cheni.