Sunday, February 1, 2015

"IYOBO HAJANIPA MIMBA.... NIKIJIFUNGUA NTAMTAJA BABA WA MTOTO WANGU.. "....AUNTY EZEKIEL

KAMA kawaida wadau wa safu bora kabisa ya
Sindano Tano, kutokana na maombi yenu leo
tumemleta yule mwanadada kipenzi cha wengi
Aunt Ezekiel amefungukia maswali matano .
Mwanadada kipenzi cha wengi Aunt Ezekiel .
Paparazi: Mambo vipi ? Kwema lakini Aunt?
Ehne leta maneno, mna mipango gani na baba
mtoto mtarajiwa , Iyobo?
Aunt: Hahaha mimi mzima! Kuhusu Iyobo,
mh! Kanipa mimba ! Si kweli , nitakapojifungua
nitamtaja baba wa mtoto wangu.
Paparazi: Mbona Iyobo amekuwa akijinadi
kwenye vyombo vya habari kuwa mzigo
ulionao ni wake ?
Aunt: Mh! Jibu langu ni hilo nililokupa .
Paparazi: Msanii gani wa kike ambaye
unamkubali sana Bongo.
Aunt: Kwa kweli namkubali sana Wema
Sepetu.
Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyobo.
Paparazi: Hivi kabla ya kuingia kwenye ‘ u -
miss ’ ulikuwa unafanya shughuli gani ?
Aunt: Nilikuwa nishaanza uigizaji ndipo
waandaaji wa mashindano ya u-miss
waliponiona na kuniambia nafaa na baada ya
hapo nikashiriki kule Ilemela , Mwanza .
Paparazi: Ukiambiwa utoe ushauri juu ya penzi
la shemeji yako wa zamani Diamond kwa
mpenzi wake wa sasa Zari , utawaambiaje ?
Aunt: Hahaha ! Jamani hapo kwa kweli ‘ no
comment ’ .
Ukitaka msanii yeyote atoke kwenye safu hii
tuma jina lake kupitia namba 0716 - 506225 .