Juma Nature ana wasiwasi kuwa itafika wakati wasanii kama yeye watapotea kutokana na kutopewa nafasi katika mambo mbalimbali.
Nature ameiambia Paparazi kuwa wadau wa muziki na vikundi vya watu vimekuwa vikiwatumia wasanii wa aina moja kila siku na hivyo wasanii wengi akiwemo yeye kutoonekana kabisa.
“Muziki unakuwa lakini kuna wasanii wanabaki pala pale,” amesema Nature. “Wachache ndo wanapata mashavu. Hebu muangilie kama Rich Mavoko ana tatizo gani? Watu wanawatumia wasanii wa aina moja na ndo hao wamekuwa wakiwasapoti na kuwaacha wasanii wengine wakiwa hawana issue.
Sasa wewe unategema nini? Kila siku Diamond, Diamond, Diamond kwanini isiwe na Ali KibA au wasanii wote wapewe fursa sawa ili tufike mbali? Mimi sitaki kumlaumu mtu ninachotaka kusema ni kila msanii apewe nafasi,” amesisitiza rapper huyo.
“Unajua wakati sisi tupo Bongo Record, wasanii wote tulikuwa wamoja/ Show tunafanya kwa pamoja na tunagawana kile kinachopatikana kila mtu anaridhika. Sasa hivi muziki umebadilika kabisa, wachache wananufaika na wengine wanaendelea kupotea. Wewe ujiulize wasanii wakongwe wote wapo wapi? Wanapotea.”