Thursday, February 12, 2015

KIBAKA WA BODABODA AFA KWA KUCHOMWA MOTO DAR KWA KUIBA MKOBA

Mwendesha bodaboda akiendelea kuteketea kwa moto baada ya kuchomwa na wananchi wenye hasira katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam,  juzi jioni ambapo alidaiwa kumpora mkoba dada mmoja na kujaribu kukimbia.
Wananchi wenye hasira  katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam,  juzi jioni walimchoma moto mwendesha bodaboda aliyekuwa amempakiza mwenzake ambao wanadaiwa kumpora mkoba dada mmoja na kujaribu kukimbia.
Wawili hao wakiwa kwenye harakati kukimbia wananchi hao waliwazingira ambapo aliyepakizwa aliruka na kufanikiwa kukimbia lakini aliyekuwa akiendesha alidhibitiwa na kupewa kipondo kikali na kuchomwa moto na bodaboda yake.