Wednesday, February 11, 2015

NIGERIA WASIKITIKIA FILAMU YA EXPENDABLES YA TANZANIA, WASEMA KAMA INGEFANYWA NCHINI HUMO MANAIKI SANGA ANGEKUWA SIO MWENZETU TENA...!


Na Mwndishi Wetu  
Nyota wa filamu nchini Nigeria wamempongeza msanii wa filamu nchini Tanzania Manaiki Sanga " The Don" kwa kuandika historia mpya Tanzania kwa kufanya filamu kubwa na ya kwanza nchini ya Expendables au Wake Up.
Lakini hata hivyo katika taarifa hizo toka kwenye mtandao mmoja wa wasaniii wa filamu nchini humo wenye muunganiko na mtandao wa Filamu Central wa Tanzania unamilikiwa na mdau wa filamu za Kitanzania Mfwahisa Georg. walisema kuwa wanamsikitia msanii Manaiki Sanga kwa kutumia mamilioni ya shilingi kuandaa filamu hiyo ambayo hata nchini Nigeria haijawahi kufanywa lakini huenda asipate faida kubwa kutokana na Kampuni nyingi za usambazaji filamu Tanzania kuwa wanyonyaji.
Wasanii hao waliendelea kusema kimsingi ingekuwa kama Manaiki Sanga ndiyo mnigeria na amefanya filamu hiyo nchini humo basi leo hii angekuwa bilionea kwa kazi yake hiyo nzuri.
Filamu hiyo iliyowashirikisha wasanii kama Irene Uwoya, Jackline Wolper, Gabo, Othuman Amri “King Majuto” Kajala, Yusuph Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed Suleiman, Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul, Flora Mvungi, Tracy Moshi, Hemed Kavu “HK” kwa upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B, Kiss, Juta B, akiwemo mwenyewe Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa filamu hiyo na wengine wengi huku ikielezwa kwamba filamu hiyo ipo kwenye biashara kwa wadosi wa Spets .Credit: maskanibongotz