NYOTA wa filamu na muziki nchini, Isabela Mpanda ambaye ni maarufu kama Bela, hivi karibuni alijikuta katika majonzi baada ya kijana wake wa kiume kuwasha moto na kuunguza godoro na ukuta wa sehemu ya nyumba aliyopanga.
Godoro la Nyota wa filamu na muziki nchini, Isabela Mpanda likiwa limeteketea kwa moto.
Risasi Mchanganyiko lilimkuta msanii huyo akiwa amejiinamia nyumbani kwake muda mfupi baada ya majirani kumsaidia kuzima moto huo.
Ukuta wa nyumba aliyopanga Isabela Mpanda ukiwa umeungua kwa moto.
“Yaani sijui mtoto huyu kwa nini ananirudisha nyuma kwa sasa nina hali ngumu hivi afu ananiunguzia godoro, nitatoa wapi hela ya kununua lingine kwa sasa?” alisikika akilalamika msanii huyo na kuongeza kuwa licha ya kulazimika kununua godoro lingine, pia atatakiwa kutengeneza sehemu ya ukuta ulioungua.