KWAKO mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’. Mambo vipi? Mishe zinasemaje? Binafsi mimi ni mzima wa afya, maisha yanasonga mbele kwa kasi ya ajabu. Tunapambana!
Nimekukumbuka leo kwa barua maana kitambo kidogo hatujaonana. Nakupongeza kwa nyimbo zako maana hata wale waliosema ulibebwa na Diamond katika wimbo wa Muziki Gani, sasa hivi wanajutia kauli zao.
Wanaona walikosea maana umefyatua nyimbo zako mwenyewe na unaendelea kukimbiza mitaani.
Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukueleza kwamba wewe ni staa hivyo unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kila mtu katika jamii. Hutakiwi kuteleza hata kidogo. Ukiwa wewe ndiyo kinara wa majanga, utatolewa mfano kwamba hufai kuigwa kutokana na matendo yako maovu.

Kila mmoja anatambua uwezo wako, anatambua hatua ambayo umefikia kimuziki. Watu wanatambua kwamba una mchumba ambaye una mikakati ya kufika naye mbali kwa maana ya ndoa Mungu akipenda.
Kinachoshangaza ni kwamba, inakuwaje unaonekana katika pozi za kimahaba na mwanamke mwingine? Picha zenyewe zinatia kinyaa?
Mwishoni mwa wiki iliyopita gumzo katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni wewe na picha zako za utupu na mwanamke huyo ambaye hakuwa mchumba wako.Ndugu yangu, picha zile hazikuwa nzuri kwako. Zimekudhalilisha na hata kukuletea ugomvi kwa mchumba wako.
Kwa nini ulikubali kupiga picha za namna ile? Zilikuwa za nini? Ulikuwa na malengo gani? Hata kama mlikuwa katika ‘shooting’ ya wimbo kwa nini ulikubali kupigwa picha katika hatua ile?
Tena bora zingevujishwa na mtu mwingine, wewe mwenyewe unatajwa kuwa ndiye chanzo cha kusambaa kwa picha hizo kupitia mitandao yako ya kijamii, hivi kwenye kichwa chako uliwaza kabla ya kufanya?
Tena bora zingevujishwa na mtu mwingine, wewe mwenyewe unatajwa kuwa ndiye chanzo cha kusambaa kwa picha hizo kupitia mitandao yako ya kijamii, hivi kwenye kichwa chako uliwaza kabla ya kufanya?
Unapaswa kujiheshimu hata kama ni video ya wimbo, naamini kwa desturi zetu, kamwe huwezi kuruhusiwa kurusha video ya namna hiyo hewani. Tamaduni zetu haziruhusu, unasubiri nani akuzuie kufanya hivyo wakati wewe kama kioo cha jamii unapaswa kuwa mfano?
Una watoto sasa, ulimwengu wa sasa si ule wa zamani. Picha zako za utupu zinachapishwa magazetini, zitasambaa kwenye mitandao mbalimbali na wanao pia watajionea bila wasiwasi. Watajifunza nini kutoka kwa baba? Jibu najua unalo na haliwezi kuwa zuri kwa mtu muungwana.
Ulimwengu wa sasa, ukifanya vituko vya namna hiyo, rekodi zake zinabaki kwenye mitandao. Vizazi na vizazi vitakuja kuona hayo uliyoyafanya juzi. Badilika kaka!Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa, kwa leo naishia hapa, naamini utafanyia kazi mawazo yangu na kubadilika.
Wasalaam,
Wasalaam,