Hii bado ni story ambayo imeendelea kukaa kwenye headlines, siku chache zimepita tangu Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aanguke kwenye ngazi akiwa anashuka baada ya kuhutubia wananchi na wanachama wake.
Story ziliendelea mitandaoni kuijadili ishu hiyo, watu wa graphics nao wakatengeneza picha mbalimbali za kuchekesha kitu ambacho kiliwakwaza viongozi wa chama cha ZANU-PF.
Leo vyombo vya habari Zimbabwe vimeripoti kuhusu Rais huyo kuwatimua kazi wafanyakazi 27 kwenye kikosi cha Usalama kwa kushindwa kuwajibika wakati Rais huyo akianguka.
Uzembe ambao unaonekana kufanywa na jamaa hao ni kitendo cha kushindwa kumdaka kiongozi huyo wakati akianguka, kibaya zaidi ni kwamba alianguka mpaka chini bila msaada wowote kutoka kwao huku wakiwa wamesimama pembeni yake.
Vingine ambavyo huenda hatukuwahi kuvisikia kuhusu ishu hii ni kwamba waandishi waliopiga picha wakati Rais huyo akianguka walilazimishwa na walinzi wa Rais kufuta picha hizo.
Taarifa za kutoka Ikulu ya Rais huyo zinasema huu ni mwanzo tu, uchunguzi unaendelea na wakipatikana wazembe wengine nao watawajibishwa kama walivyofanyiwa hapa.
Hii ni video ikionesha Rais huyo wakati akianguka huku walinzi wake wakiwa pembeni yake.