Thursday, February 5, 2015

VIDEO inayoonyesha Rais Mugabe akianguka kwenye ngazi

Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe tumesikia mara nyingi akiwa na migogoro na mataifa ya Ulaya, Marekani ishu kubwa ni kitendo cha Mugabe kuonekana akiendelea kung’ang’ania madaraka kwa kipindi kirefu.
Video, picha na story kubwa mitandaoni kwa sasa ni ishu ya Rais huyo kuanguka wakati akishuka ngazi baada ya kuhutubia wanachama wake Harare, baada ya kumaliza kuhutubia alisalimiana na viongozi kadhaa wa Chama hicho halafu akawa anashuka ngazi, akaishiwa nguvu na kuanguka chini, walinzi wakamuinua na kumpeleka kwenye gari yake.
Mugabe-7
Kwenye video Mugabe anaonekana akishuka ngazi lakini hali yake ni kama mgonjwa au mtu aliechoka.