Monday, February 9, 2015

Wema Sepetu Khaaa! Aenda South Africa kula Bata na Aliyekuwa Mume wa Zari ‘What Goes Around Comes Around'

Kuanzia Kulia: King Lawrence, Ivan Ssemwinga na Wema Sepetu
Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zari The Bosslady na aliyezaa naye watoto watatu ameanza kurusha mashambulizi kwa adui yake namba moja, Diamond Platnumz....



Mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini huenda akalipiza kisasi kwa Diamond anayetarajia kupata mtoto wake wa kwanza kutoka kwa Zari kwa mbinu ya ‘jino kwa jino’ ama zile za ‘kama noma basi iwe noma’.

Picha liko hivi, Wema Sepetu kumbe yupo nchini Afrika Kusini ambako hata hivyo hatufahamu ameenda kufanya nini. Mshkaji wa karibu wa Ivan, King Lawrence (Yule mchizi aliyempa ofa Diamond ya $40,000 ili aachane na Zari), ameshare picha kwenye mtandao wa Instagram akila bata na Wema huku Ivan akiwpo pia.
Wema, Ivan na Lawrence akiwa na demu wake

Kwenye picha hizo, Lawrence anaonekana akiwa amekaa juu ya mapaja ya msichana asiyejulikana na pembeni yake yupo Ivan huku Wema aliyevaa kigauni kifupi cheusi akiwa kulia kwake.

Lawrence pia amepost video kadhaa akiwa kwenye club hiyo na kuziandika ujumbe wa mfumbo ambao unaeleweka wazi kuwa unawaendea Zari na Diamond. “Rich Gangstas – What goes around comes around,” ameandika. “Oh Z*** get out of the way,” ameandika kwenye video nyingine ambayo unasikika wimbo wa Ludacris, Move Bitc*.

Awali Lawrence alipost picha nyingine hiyo chini akiwa kwenye eneo lile lile ambalo Wema alipiga picha.

Ni mapema sana kuhitimisha kuwa Ivan anataka kulipiza kisasi kwa Diamond kwa kumchukua Wema, lakini ni wazi kuwa kambi yake inataka kupeleka ujumbe ulio wazi kwa Chibu kuwa ‘vita imeanza’.

Acha project iendelee…