Friday, March 27, 2015

NYUMBA YA RUBANI WA NDEGE YA GERMANWINGS YACHUNGUZWA

Mabaki ya ndege ya Ujerumani ilioanguka na kuwaua watu 150
Chumba cha rubani wa ndege.
Baada ya kufanya msako katika nyumba yake. Polisi nchini Ujerumani wamegundua kile wanachosema kitawasaidia katika kubaini kiini cha rubani msaidizi Andreas Lubitz, kuangusha ndege na kuwauwa abiria wote 150.
Polisi hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana na kile walichokipata, lakini baadhi ya vitu vyake vikiwemo Kompyuta, vimechukuliwa ili kuchunguzwa.
Huku uchunguzi huo ukiendelea, imebainika kuwa rubani huyo alitatiza kwa muda, mafunzo yake ya urubani mwaka 2008, kutokana na kutibiwa matatizo ya kiakili.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ujerumani, Tomas de Maiziere, anasema kuwa, uchunguzi wa kiusalama dhidi ya rubani huyo, haujasema lolote huku, muajiri wake kampuni ya Lufthansa, ikisizitiza kuwa Lubitz alikuwa asilimia mia kuendesha ndege.