Monday, April 13, 2015

Baada ya WEMA kufunguka Juu ya Kutoweza kupata MIMBA: Riyama Ampa Wema Neno la Faraja na Matumani

 Baada ya hapo jana Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu kueleza kuwa anatamani sana kupata mtoto lakini hana uwezo huo,Staa mwenzake ambae ni mama wa mtoto mmoja, Riyama Ally ampa neno hili la faraja na matumani.


“Naomba hapa unisikie kwamakini nabii ibrahim alimpata na bii ismail akiwa na umri mkubwa sana utuuzimani wema bado mdogo muda utafika inshallah mola atakupa mume mwenye kheri na wewe uzae jike na dume usiumie mama mungu hukupa akujaalialo na sio umuombalo watoto ni kudra za mola na sio jitihada za wana dama atakupa maa muda ikifika tena utapakata na utanyonyesha inshallah amin nakupenda sanaaaaaaaaaa”- Riyama ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandaoni. mara baada ya kubandika picha ya Wema.