Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 nipo ofisini na naanza kupokea simu nyingi za watu wangu wakitaka kujua ukweli kuhusu taarifa zilizoenea kwamba msanii wa bongoflevaHussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.
Baada ya hapo naanza kupiga simu ya Hussei Machozi inaita lakini haipokelewi kwa zaidi ya nusu saa, naanza kupata wasiwasi, nikiwatafuta rafiki zake pia sifanikiwi lakini baadae naendelea kuipiga simu ya Hussein na inapokelewa.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe, anaanza kwa kusema ‘Nilijiandaa hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana, msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipoDar es salaam‘
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Sasa hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.
Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…
habari hii ni kwa mujibu wa millardayo.com