Monday, April 6, 2015

LORI LAFELI BREKI NA KWENDA KUGO GA PRADO... TAZAMA HAPA

Lori la Mizigo lenye namba za usajili T
255 CRN na lililokuwa na Tela lenye
namba za usajili T 478 BCG likiwa
limefunga njia baada ya kufeli breki lilipo
kuwa kwenye njia kubwa katika eneo la
Mbezi Mwisho, Jijini Dar es salaam. Kwa
mujibu wa Dereva wa Lori hilo
aliejitambulisha kwa jina moja la Bw.
Sendegwa, alisema kuwa alianza safari
yake ya kutoka Mkoani Singida akiwa
vizuri kabisa na alipofika maendeo ya
Kibamba alihisi gari yake kupoteza upepo
lakini kwa wakati huo alikuwa kwenye
mwendo mdogo tayari na alianza
kujarubu kutafuta namna ya kusimama
lakini hakufanikiwa, na alipofika maeneo
ya Mbezi aliona sehemu ya kuchepuka
ambayo aliona ni salama kwa upande
wake na ndipo alipoamua hivyo na huko
alikutana na Gari dogo aina ya Toyota
Prado lenye namba za usajili T 902 DCS
ambapo alilipiga pasi ubavuni na kwenda
kukita kwenye baraza la moja ya nyumba
zilizokuwepo kwenye eneo hilo.
Hakuna aliejeruhiwa wala kupoteza
maisha kwenye ajali hiyo.