Nay wa Mitego ni mtu wa maamuzi na mapenzi tofauti na wengine. Ndio
maana ukiingia ndani kwake utakutana na sanamu isiyo ya kawaida – ni
sanamu ya shetani!
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa sanamu hiyo ni moja ya vitu anavyovipenda zaidi ndani mwake.
“Mimi naipenda na niliinunua hela nyingi tu, ni dola elfu tatu,” amesema Nay.
“Nilitokea tu kuipenda, ni moja kati ya vitu muhimu ninavyovipenda ndani
ya nyumba yangu. Kuna sehemu niliinunua sio Tanzania. “Mimi nilitokea
kukipenda yaani naipenda sana tena sana na hata ukiingia ndani kwangu
utaanza kuiona hiyo,” amesisitiza rapper huyo.