Tuesday, May 12, 2015

AMBER ROSE AVUJISHA SIRI ZA KANYE WEST

Mwanamitindo, Amber Rose.
Los Angeles, Marekani
KIMENUKA! Ndiyo neno sahihi unaloweza kulitumia baada ya mwanamitindo, Amber Rose, kuanza kuvujisha siri za aliyekuwa mpenzi wake, Kanye West.Katika siku za hivi karibuni, uhusiano kati ya Amber na Kim Kardashian ambaye ndiye mke wa sasa wa Kanye, umekuwa siyo mzuri na wamekuwa wakipigana vijembe, jambo linaloonekana kumshawishi Amber kuanza kutupa madongo.
Kanye West.
Amber, 31, ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alitoa siri hiyo hivi karibuni akiwa katika klabu ya usiku ya Supper Club, Los Angeles, ambapo alidai Kanye kwa muda mrefu amekuwa akiandikiwa mashairi yake na hawezi kuandika mwenyewe.
Amber alifikia hatua hiyo baada ya kupigwa ngoma ya Kanye kwenye klabu hiyo. Alisikika akisema: “Mnadhani sifa anazopata anastahili, kuna watu watabisha lakini mimi ndiyo nilikuwa ninaishi na Kanye, najua mambo mengi juu yake, nyimbo zake nyingi alikuwa akiandikiwa na kijana mdogo, Travis Scott.”
Kabla ya kufunga ndoa na Kim Kardashian miezi 23 iliyopita huku wakifanikiwa kupata binti yao North West, Kanye alikuwa na uhusiano na  Amber tangu mwaka 2008 mpaka mwishoni mwa mwaka 2010.