Tuesday, May 12, 2015

BAADA YA KUPIGWA CHUPA, KAJALA ASEMA MAISHA YANAENDELEA

Kajala Masanja akiwa na bandeji kichwani baada ya kupigwa chupa.
STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja, kupitia akaunti yake ya Instagram hivi punde amesema maisha yanaendelea ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa chupa na mtu asiyemfahamu usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa klabu wakati alipokwenda katika shoo ya kumchangia mke wa Mabeste, Maisha Club.
Kajala akiwa Maisha Club kabla ya kujeruhiwa kwa chupa. 
Kajala alieleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati akijiandaa kutoka Maisha Club ambapo ghafla akiwa kwenye ngazi alirushiwa chupa kichwani iliyopelekea kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamalia wema waliompeleka Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa kwenye jeraha alilolipata.
Staa huyo aliongeza kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa  hamjui na wala hajawahi kumuona mtu huyo.