Mmiliki wa klabu ya Tiger Lounge, Thadei Chusa ‘Tiger Man’.
BILIONEA mdogo kutoka Mirerani anayejulikana kwa jina la Thadei Chusa ‘Tiger Man’ amezindua Tiger Lounge ya mastaa wa Bongo Movies ili wawe na sehemu ya kupumzikia na kutafakari jinsi ya kuendeleza sanaa hiyo.
Alisema club hiyo itakuwa pia ni kwa ajili ya watu wengine ambao watapenda kuja kuonana na mastaa hao hapa Bongo na kutakuwa na siku yao maalum ya kukutana na kufanya vitu mbalimbali ambapo wakazi wa jiji la Arusha watapata fursa ya kupiga nao stori mbalimbali.