Wednesday, May 20, 2015

HATARI! KINYESI CHA PANYA, MKOJO WA BINADAMU VYATUMIKA KWENYE VIPODOZI

Kinyezi cha panya na mkojo wa binadamu ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeza bidhaa ghushi za urembo.
Je wewe ni mnunuzi wa bidhaa za urembo? Tahadhari.
Kinyesi cha panya na mkojo wa binadamu ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeza bidhaa ghushi za urembo.

Utafiti wa bidhaa za urembo zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza umebaini kuwa bidhaa hizo zina tengezwa kwa njia isiyofata maadili na kulinda afya ya binadamu.
Utafitri huo uliochunguza bidhaa za urembo kama vile vipodozi marashi na mafuta ya kujipaka iligundua kuwa zinaongezwa madini ya sumu kama vile arsenic.
Kwa mujibu wa Polisi waliotekeleza uchunguzi huo, mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki kumechangia pakubwa ongezeko la mauzo ya bidhaa gushi.
''ni vigumu sana kubaini uhalali wa bidhaa haswa unaponunua kwa njia ya kielektroniki kwa sababu unachokiona hapo mtandaoni ni picha tu ya bidhaa halali''
''sasa bidhaa hiyo inapokufikia huwa tayari umekwisha lipia na ni vigumu sana kwako kurejesha bidhaa hizo pindi unapokuwa hujaridhia ubora wake'' alisema afisa aliyesimamia uchunguzi huo.
Marashi mengi yanamkojo wa binadamu na sumu ya arsenic
Bidhaa za kielektroniki zinazopendelewa na wafanyibiashara walaghai ni kama zile zile zinazosokota nywele na pia zingine zinazotumika kwa ususi.
Hata hivyo bidhaa hizo haziwezi kuhimili matumizi ya muda mrefu na hivyo zinahatarisha maisha ya watumizi kutokana na hatari kulipuka.
Isitoshe Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa marashi ghushi yanayouzwa London yanajumuisha sumu aina ya Cyanide na mkojo wa binadamu.
Vipodozi vimepatikana na sumu aina ya arsenic madini yenye sumu ya zebaki na risasi .
Vipodozi hivyo vinaweza kusababisha kujikuna,vipele visivyokwisha na maradhi mengine ya ngozi.
Bi Maria Woodall, anayeongoza kitengo cha uchunguzi wa hati miliki ya bidhaa alionya kuwa watu wengi hawafahamu madhara ya kutumia bidhaa ghushi.
CREDIT: BBC