Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa ameshika tuzo yake.
MKURUGENZI wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina yake baada ya kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper, Elizabeht Michael ‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu.
Wadau mbalimbali waliohuzuria wakufuatilia hafla hiyo ya utoaji tuzo. Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei, 23 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.Wema aliibuka kinara na kuwafanya baadhi ya mashabiki wake walipuke kwa shangwe huku Wolper, Lulu na Riyama wakibaki kimya.
Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa na Meneja wake Martin Kadinda. Akizungumza kwa furaha muda mfupi baada ya kutwaa tuzo hiyo, Wema alisema kwamba amefurahia kuwa mshindi na amejisikia vizuri kwani hakutarajia kuibuka kidedea, ila anaamini mashabiki wake ndiyo waliomfanya akashinda na kuahidi kuwa nao bega kwa bega.
“Nashukuru sana kwa kutwaa tuzo hii ambayo kwa namna moja au nyingine naiona kama sapraizi maana tulikuwa tukigombea wengi, ila mashabiki wangu wameniwezesha kwa kiasi kikubwa kuitwaa tuzo hii, ninachoweza kusema kwa sasa nashukuru sana uongozi wa Endless Fame hususan meneja na wafanyakazi wangu wote,” alisema Wema.