Monday, May 11, 2015

HOFU: CHATU AMMEZA MBUZI MZIMAMZIMA, WANAKIJIJI WAPIGWA BUTWAA

Chatu akimmeza mbuzi katika Kijiji cha Garkhuta, India.
TUKIO la chatu mwenye urefu wa futi 10 akimmeza mbuzi mzimamzima limewatia hofu wakazi wa Kijiji cha Garkhuta kilichopo Magharibi mwa Bengal nchini India.
Tukio hilo lilinaswa na Mpigapicha, Roni Choudhury hivi karibuni wakati akitembea jirani na Hifadhi ya Msitu wa Sonakhali nchini India.
Kitendo hicho kiliwafanya wanakijiji waingiwe na hofu huku Ofisa Misitu wa Wilaya, Vidyut Sarkar akisema kuwa: 'Iwapo chatu huyo alimkamata mbuzi, anaweza pia kumuua hata mwanaume au mtoto'.
Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi ambao hawakuonyesha kumuogopa sana chatu huyo aliyekuwa akimmeza mbuzi na badala yake kushuhudia tukio zima. Ilimchukua chatu huyo saa nne kummeza mbuzi huyo.