Wednesday, May 20, 2015

Ilikuaje siku Ney wa Mitego alipomtanguliza Stan Bakora kwenye show?

stan 
Stan Bakora kwa sasa yuko kwenye headlines  za wachekeshaji ambao wanapendwa kulingana na vichekesho vyao Tanzania,yeye vichekesho vyake anafanya na Rafiki yake Kitale ‘Mkude Simba‘
Style anayotumia Stan Bakora kuchekesha ni ile ambayo anaonekana anajibishana na Kitale lakini kwa lafudhi ambayo kama ukimsikia vibaya unaweza kuhisi ni Rappa Ney wa Mitego.
Ney wa Mitego na Stan Bakora kumbe wanafahamiana siku nyingi leo Stan anatupa stori kuwa kuna siku ambayo Ney wa Mitego alichelewa kwenda kwenye show akawa amewatanguliza Stan Bakora na wenzake ili wahusika waamini kuwa atafika.
Walipofika mkoa ambao Ney alikua anafanya show wakati wanatoka hotelin wakati anaongea wakamuuliza ‘Wewe ndio Ney?’ anasema aliogopa kujibu ndiyo yeye kwa sababu alikua na hofu ya kupigwa akawajibu ‘Ney mwenyewe anakuja‘