Dominyk Alfonseca kutoka Virginia Beach, Marekani ana kesi ya kuvamia Benki na kuiba dola 150,000 lakini akaona watu wake wasipitwe, akarekodi tukio zima alafu akapost kwenye ukurasa wake wa Instagram!! Dakika kama 20 baadae akakamatwa na Polisi !!
Dominyk mwenyewe ana ndoto za kuwa rapper.. baada ya kukamatwa na Polisi alijitetea kwamba anashangazwa na watu wanavyomuita mwizi kwani kwenye karatasi ya ujumbe aliompatia teller wa benki hakuomba pesa hizo kwa nguvu bali aliomba tu taratibu bila kutumia nguvu na akapewa.
Kwenye utetezi wake jamaa anasema hivi; “Sijui kwanini wananiita mwizi.. mimi nilisema “naomba” sikutumia nguvu.. angesema hapana au sitaki mimi ningeondoka zangu tu bila matatizo“– Dominyk Alfonseca.