Monday, May 11, 2015

KIOJA..!! HII NDIO HOTELI KWA AJILI YA WATU WANAOTAKA KULIA NA KUTOA MACHOZI

lia
Inaweza hii ikakushangaza kidogo lakini huu ndio ukweli baada ya hotel moja mjini Tokyo Japan kuamua kuwatengenezea vyumba maalum wanawake kwa ajili ya kulia.
woman
Mmoja wa wanawake akiwa ndani ya vyumba hivyo
Hotel hiyo inayojulikana kwa jina la Mitsui Garden Yotsuya  inasemekana imeamua kufanya hivyo ili kuwaruhusu wanawake  wageni wanaokuja hapo kulia wakiwa huru tena kwenye mazingira mazuri ambayo hayawezi kuwasumbua.
cry
Unaambiwa ndani ya hotel hizo kuwa vitambaa kabisa vitakavyotumika kufuta machozi pamoja na ‘makeup’ vipozodi ambavyo watatumia baada ya kukata kiu yao.
Pia kuna mikanda ya video yenye kusikitisha ambayo wamewekewa kwa ajili ya kuitazama ili kuwasaidia kuongeza kulia kama A moment to Remember na Forest Gump.

Gharama kwa usiku mmoja ni Yen 10,000 ambayo ni sawa na 150,000 ya Kitanzania.