Thursday, May 21, 2015

KUMBUKUMBU YA MIAKA 19 YA AJALI YA MV BUKOBA

Mnara uliopo eneo la Igoma, Mwanza kwenye makaburi ya baadhi ya watu waliokufa katika ajali hiyo.
Makaburi ya baadhi ya marehemu wa ajali hiyo yaliyopo Igoma, Mwanza.
Meli ya MV Bukoba wakati ikizama katika Ziwa Victoria na kuua zaidi ya watu 800.
NI miaka 19 imepita leo tangu Watanzania wapate pigo kubwa la kuondokewa na ndugu, jamaa na marafiki katika ajali mbaya ya majini iliyohusisha meli ya MV Bukoba.
Ilikuwa Mei 21,1996 katika ziwa Victoria, ambapo meli ya MV Bukoba iliyokuwa imejaa abiria pamoja na mizigo ikitokea mkoani Kagera kwenda Mwanza ilipozama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 800.
Meli hiyo ilizama ikiwa imebakiza kilomita 30 kutia nanga kwenye bandari ya Jiji la Mwanza.
Daima tutazidi kuwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo.