Thursday, May 21, 2015

MILLEN MAGESE KUWA MTANZANIA WA KWANZA KUPATA TUZO YA BET, UGONJWA WAKE WAMFANYA AJULIKANE DUNIA NZIMA

WaTanzania wenzangu nomba kuchukua nafasi hii kumpongeza dada yetu @ladivamillen ambaye amechanguliwa kwenda kuchukua BET Global Good Award kwenye tuzo za Mwaka huu za BET Awards Marekani. Ni category mpya ambayo haina mipaka na haina nominees kachaguliwa yeye kuwa anastahili kukabidhiwa tuzo hiyo. Lakini pia ni tuzo ya kwanza ya BET kwa Mtanzania. Ni jambo la kujivunia. Mimi nimefurahi mnooooo alivyoanza kuzungumzia ugonjwa wake kama elimu kwa wengine watu walimbeza, wako walitaka kumkatisha tamaa ila sasa ona Mungu kamwinua katambuliwa kimataifa kwa kazi zake na dunia nzima tutam-salute pia. It's always about you and your God first. God bless you my sister @ladivamillen kwanza mzuri, una moyo mzuri, moyo wa dhahabu huna shida na mtu. You are a true Tanzanian Icon. More power to you. Mungu azidi kukuinua. Nakupenda. Naomba tumpogeze dada @ladivamillen kwa heshima hii kubwa aliyopewa. Usengwile wanachama. ❤️❤️❤️ #MwanamkeWaNguvu