Thursday, May 21, 2015

MOSE IYOBO: HALI YA BEBI IMENIFANYA NISIENDE LONDON

Imelda Mtema
MPENZI wa staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel, Moses Iyobo ambaye pia ni dansa mahiri wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa hakwenda kwenye shoo iliyokuwa ikifanyika katika Jiji la London kutokana na hali ya mpenzi wake.
Staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo.
Akichezesha taya na Centre Spread, Mose alisema kuwa  alishindwa kujumuika na wenzake akihofia hali ya mpenzi wake hivyo alipenda kuwa naye karibu hadi kwenye hitimisho lake la kumpata mtoto wao.
“Unajua nashindwa kwenda mbali sana kutokana na hali ya mpenzi wangu kwa kuwa nakuwa na wasiwasi sana hivyo hata London nimeshindwa kwenda kwani natamani kuona hatua kwa hatua ya bebi wangu hadi kumpata mtoto wetu,” alisema Mose.