Thursday, May 21, 2015

JOHARI NILIKUWA MAMA NTILIE!

Brighton masalu
KABLA hajaanza ‘kuuza sura’ kwenye runinga, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’ alikuwa akijihusisha na kazi ya upishi na uuzaji wa chakula biashara ambayo aliifanya jijini Dar kabla hajajiunga na Kundi la Sanaa la Kaole baada ya kuhitimu mafunzo ya Hotel Management.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’.
Johari alianza kupika na kuuza chakula kwenye catering ya shangazi yake huku akihangaika kutafuta njia ya kutimiza ndoto yake ya uigizaji aliyokuwa nayo tangu akiwa kijijini kwao Bugoyi mkoani Shinyanga.Johari anasema aliamua kusomea masomo ya upishi kwa kushinikizwa na ndugu zake walioamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kupika chakula kizuri na kitamu japo moyoni mwake hakuwa na ‘hobi’ hiyo.
“Kabla ya kutimiza ndoto yangu hii ya uigizaji, nilikuwa napika na kuuza chakula, si unajua katika maisha kabla hujatimiza ndoto na malengo yako ni lazima uhangaike kwa kupitia vikwazo na vizingiti vingi?
“Hivyo mimi nilijikuta nikiangukia kwenye u-hotelia japo sikuwa interested kabisa, lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwa kuwa nimetimiza ndoto yangu,” alisema Johari katika mahojiano maalum na mwandishi wetu hivi karibuni.