Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena,alisema kilichomtokea Diamond hata yeye kilimtokea wakati alipotoa wimbo wake wa ‘Bado Nipo Nipo Kwanza’ ulifanya vizuri wakati huo lakini jina lake halikuwepo kwenye tuzo hizo.
Mwana FA |
‘’Hata mimi nililalamika kama anavyolalamika Diamond lakini niliwaandikia barua Killi wakaniita wakanielewesha kuwa ilikuwa ni makosa ya kibinadamu nikaelewa,’alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo amesikitishwa na wasanii Mo Music na Ommy Dimpoz kutokuwepo kwenye tuzo hizo hasa video ya ngoma ya Ndagushima ambayo ilifanya vizuri mwaka jana.
Diamond amelalamikia kutokuwepo kwenye kipengele cha msanii bora wa mwaka,na bendi ya Yamoto kufanya vyema mwaka jana lakini imepata nafasi finyu kwenye tuzo hizo.