Staa mkali wa sinema za Bongo, Wema Sepetu.
KWELI dhamira inauma! Staa mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ameamua kukifungua kinywa chake na kusema kuwa anamwomba msamaha zilipendwa wake katika urafiki, Wema Isaac Sepetu kwa mabaya yote aliyomtendea, Amani linakupa zaidi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mapaparazi wetu mapema wiki hii jijini Dar, Kajala alisema hata kama kuna chuki ya ukubwa kwa kiasi gani baina yao lakini Wema atabaki kuwa mtu muhimu sana katika maisha yake mpaka atakapoaga dunia!
“Najua mimi na Wema hatuko sawasawa. Lakini namwomba anisamehe sana. Naumia kila siku. Yeye ni mtu muhimu sana katika maisha yangu. Atambue hilo,” alisema Kajala.
Akizungumzia umuhimu wa Wema kwake, Kajala alisema:
“Kwanza iweleweke kwamba, namchukulia ni mtu muhimu kwa vile hakukuwa na mwingine wa kunitolea zile shilingi milioni 13 kule mahakamani (Kisutu).“Bila Wema mimi leo hii ningekuwa natumikia kifungo cha miaka 7 jela, lakini kutokana na huruma yake alinisaidia hivyo ataendelea kuwa mtu muhimu sana kwangu.”