Friday, May 29, 2015

Odama."Siwapendi Marafiki wa Kiume Kwani Ukitaka Kitu Kwao wakusaidie lazima Nao Watake Kitu Kutoka Kwako..."

Odama Katika Pozi
Staa wa Bongo Movies,  mwenye mvuto  wa aina yake, Jennifer Kyaka ‘Odama’, amesema anaogopa marafiki wa kiume kwa kuwa huwa na masharti magumu pindi wanapotoa msaada.

Wasanii wa kiume kwangu sipendi kwa kuwa huwa na masharti kuliko marafiki wa kike ambao husaidia bila masharti ya ajabu,” alisema.

Odama Bongo Movies
Aliongeza kwamba, marafiki wa kike anakuwa huru kuwaeleza shida na matatizo yake kuliko wa kiume ndiyo maana hiyo ni sababu yake nyingine ya kutopenda marafiki wa kiume kama anavyopenda marafiki wa kike.