Walemavu wakiwa wamekaa barabarani wakati wa maandamano hayo.
Wananchi wakitaharuki kufuatia maandamano ya walemavu kuelekea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya walemavu wakihojiwa na waandishi wa habari.
WALEMAVU jijini Dar es Salaam leo wameandamana kwenda Ofisi za Mkuu wa Mkoa zilizopo Ilala jijini Dar na kufunga barabara za Kawawa na Uhuru wakilalamikia kuvunjwa kwa meza zao za biashara zilizopo eneo la Karume.
Maandamano hayo yalisababisha msongamano mkubwa wa magari na kupelekea usumbufu mkubwa kwa abiria na madereva waliokuwa wanatumia barabara hizo.