Friday, May 22, 2015

WAKATI WA KINA DE GEA WAKIPEWA OFA YA £250,000, HUYU JAMAA KASAINI £ 641,000 KWA WIKI

POND
Wakati wakina De Gea wakipewa ofa ya 250,000 lakini bado hawasomeki kama watasaini mkataba au la. Mwenzao kwenye michezo anavuta mpunga mrefu hatari.
Huyu jamaa ni bingwa wa dunia kwenye Formula 1 mara mbili. Lewis Hamilton amejizolea mashabiki wengi sana kutokana na life style yake kwa kujichanganaya na watu wengine maarufu wa magharibi.
Lewis amesaini mkataba na Mercedez kwa muda wa miaka 3 na kwenye huo mkataba kila wiki atakua analipwa pound 641,000. Kwa ufupi ni kwamba kwa mwaka atalipwa pound 33,333,333, kwa wiki ni £641,026, kwa siku ni £91,575 na kwa kila race atalipwa £1,571,429 .
F1