Wednesday, May 20, 2015

YULE MZEE ALIYEOA KIBINTI KIDOGO.. AFUNGUKA MAZITO HII NDIYO SIRI YA MAPENZI YAO

Gavana wa jimbo la Edo la nchini Nigeria, Adams
Oshiomhole, amemuelezea mke wake, Iara, kama
mlimbwendwe kwenye moyo wake na kwamba si
kwamba hajamuoa kuziba pengo la mke wake
aliyefariki.
Akiongea kwenye misa ya shukrani kwenye kanisa
la Immaculate Conception Cathedral, Auchi,
Jumapili iliyopita, Oshiomhole alizipuuzia ripoti
kuwa mke wake ni model maarufu na kudai kuwa
maneno hayo yametokana na urembo wa mke
wake.
“Ninaposoma habari za kwenye magazeti na
wanasema kuwa Comrade ameoa ‘mlimbwende’
mimi nasema labda ni mtu mwingine,” alisema.
“Msichana ambaye Mungu amleta kwangu kumuoa
hakuwahi na si mlimbwende. Of course, ni
mrembo na naelewa kwanini watu wanadhani
msichana wa aina hii anaweza kuwa model, of
course, ni model moyoni mwangu na tuna tumaini
na kuomba kwenye moyo wa Mungu wetu na
nadhani hicho ndio kitu muhimu.”
Gavana huyo ana umri wa miaka 63 huku mke
wake huyo mpya ana miaka 36. Mrembo huyo ni
raia wa Cape Verde na alifunga naye ndoa weekend
iliyopita.
Ndoa yao ilifungwa mbele ya wageni akiwemo rais
wa Nigeria Muhammadu Buhari na mtu tajiri zaidi
Afrika, Aliko Dangote.
Ndoa hiyo imekuwa gumzo kwenye bara zima la
Afrika.