Monday, June 15, 2015

BAADA YA VANESA MDEE SASA VIATU VIREFU VYAMUUMBUA KIM KARDASHIAN


Staa hot, modo wa ukweli, Kim Kardashian. New York, Marekani
STAA hot, modo wa ukweli, Kim Kardashian, almanusura aanguke kufuatia kiatu alichokivaa kuwa kirefu, hivyo kusababisha ajikwae, Ijumaa iliyopita huko Beverly Hills.


Kim alikwenda kufanya shopping kwenye Duka la Celine on Rodeo Drive lililopo Beverly Hills ambalo huuza mavazi ya kike, ndipo akakutwa na masaibu hayo ya kuteguka na kutaka kuanguka lakini aliweza kuhimili. Mrembo huyo ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Keeping up With the Kardashians, ni mke halali wa rapa Kanye West, sasa hivi ana mimba ya mtoto wa pili baada ya North West. Wakati akienda kujadiliana bei na muuzaji, Kim alisikika akisema: “Ooh Mungu wangu, natamani kuvitoa hivi viatu. Havinipi uhuru. Sitaki kuvivaa, nataka kuondoka ili nikavitoe.