Zimepita kama saa 48 tu toka Timu ya Yamoto Band ipae toka Uwanja wa Ndege wa JNIA Dar es Salaam kuelekea South Africa kwa kazi moja tu, kuandaa video yao ambayo wanaifanya na Director Godfather.
Picha ya kwanza ilionesha wako meza moja na Director huyo, alafu pembeni alikuwepoDiamond Platnumz pamoja na Mkubwa Fella na Babu Tale pia.
Post imepanda muda mfupi uliopita kwenye page ya Diamond @Instagram ikionesha tayari kazi imeanza… unaweza kucheki hapa kipande cha video hiyo Behind th scenesya kwanza Yamoto Band wakiwa Location.
Tunazijua kazi nzuri za Yamoto Band na tunaijua kazi nzuri pia ya Godfather, tukae tayari kwa kila kizuri kitakachotokea huko mtu wangu.