Monday, June 15, 2015

BODABODA AMSHIKA AFANDE KALIO,AKIONA CHA MOTO

Dustan Shekidele, Moro
Kibano! Mwendesha pikipiki almaarufu bodaboda aliyetajwa kwa jina la Juma Abdallah amekula kibano baada ya kudaiwa kumdhalilisha afande wa kike wa Jeshi la Zima Moto mkoani hapa, Winnifrida Kachota kwa kumshika kalio hivyo kuibua timbwili zito.
Wananchi na bodaboda wenzake waliokuwa wakimtetea mwenzao.
Tukio hilo lililoibua vita kubwa lilijiri nje ya ofisi ya Zima Moto mkoani hapa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilibidi polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuingilia kati wakiwa na silaha nzito ambapo walifyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya bodaboda hao waliokuwa wakimtetea mwenzao.
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kutuliza ghasia.
Akizungumza na gazeti hili, bosi wa afande huyo, Mkaguzi Msaidizi wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Kituo cha Morogoro, lssa lsandeka alisema askari wake alidhalilishwa kwa kushikwa makalio wakati anakatiza kwenye kijiwe cha bodaboda kuelekea kazini.
Polisi hao wakiendelea na doria.
“Alipokuja kuripoti kwetu tulikwenda kuripoti tukio hilo na sisi tulikwenda kumkamata bodaboda yule na kumpeleka polisi.“Cha ajabu, mmoja wa bodaboda alisambaza ujumbe kwa bodaboda wenzake ambao walifika hapa na kutufanyia fujo kubwa hivyo polisi wakafika na kutuliza ghasia.”
Muendesha bodaboda huyo akiwa chini ya ulinzi.
Katika tukio hilo, bodaboda hao walidaiwa kuwa walitaka kulipa kisasi kwa maafande hao wa faya huku baadhi yao wakirusha mawe kwenye kituo hicho.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mussa Mazambo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 15 kwa uchunguzi.