Wednesday, June 17, 2015
Bye bye Maisha club Osterbay! picha za Location mpya inakohamia ninazo hapa..Sasa hivi inaamia Makumbusho
Kila mmoja aliyesikia taarifa za kuhamishwa kwa NEW MAISHA CLUB alitamani kujua ni wapi itahamia kwa sababu party ya mwisho ilipofanyika walitangaza baada ya mwezi Mtukufu watu wote watahamia kwenye jumba jipya la starehe kwenye location mpya Dar es salaam.
Sasa kwa kukutaarifu tu ni kwamba location mpya ya Maisha Club ni Makumbusho nyuma ya Millenium Tower Kijitonyama Dar es salaam kwenye jengo jipya la LPF na hii itakuwa club ya kwanza Dar es salaam kuwa chini ya ardhi.
HK ambaye ni meneja wa Maisha club ameiruhusu millardayo.com kupata picha za sehemu tu ya hiyo location mpya ikiwemo Parking ya underground na nyingine ya kawaida kama zinavyoonekana na pia jengo lenyewe.
-Millard ayo