Sunday, June 7, 2015

CHRISTIAN BELLA ALIVYOFUNIKA DAR LIVE JANA

Christian Bella akiimba moja ya nyimbo zake kwa hisia.
Mashabiki wakiimba sambamba na Christian Bella wimbo wake wa Nashindwa.
Wanamuziki wa Malaika Music Band wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
Mashabiki wakipagawishwa na muziki huo.
Msanii Juma Nature, akipanda jukwaani.
Umati wa mashabiki ukimshangilia.
Hapa Christian Bella akimtambulisha Nature kwa mashabiki zake.
Christian Bella akipiga selfie na mashabiki zake.
Mashabiki wakionesha hisia zao wakati, Christian Bella akiimba wimbo wa Nani kama Mama.
SHOO ya kihistoria ya kuutambulisha wimbo wa Nashindwa kutoka kwa Mfalme wa Masauti, Christian Bella sambamba na bendi yake ya Malaika ilifanyika usiku wa kuamkia leo na kukonga nyoyo za mashabiki kibao waliofurika katika ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kushuhudia utambulisho huo.
Shoo hiyo iliyofunguliwa pazia majira ya saa 3 usiku kwa bendi hiyo kupiga vibao vyake kadhaa vya awali huku mashabiki waliowahi kufika uwanjani hapo wakipata fursa ya kushuhudia fainali ya Klabu Bingwa kati ya Barcelona na Juventus huku wakiburudishwa na nyimbo kadhaa kabla ya shoo nzima kuhamia jukwaani ambapo Mfalme wa Masauti, Christian Bella alipanda na kupiga nyimbo zake kali kama vile, Nani Kama Mama, Usilie, Wambea kisha kuutambulisha wimbo wake wa Nashindwa ambapo mashabiki waliofurika ukumbini hapo waliomba wimbo huo urudiwe zaidi ya mara tatu.
Kama hiyo haitoshi, Christian Bella alimkaribisha stejini msanii nguli wa Hip Hop, Juma Nature ambaye aliwasalimia mashabiki wake kwa nyimbo zake kadhaa kisha burudani ikaendelea na mwishowe mashabiki hao wakipata fursa ya kuitazama video ya Nashindwa iliyooneshwa kupitia ‘big screen’ iliyofungwa uwanjani hapo.