Friday, June 26, 2015

Hawa ndio waliotolewa na Ray C kwenye dawa za kulevya.Tundaman ataimba Kaswida?

26 June ni siku ya maazimisho ya kupinga dawa ya kulevya Duniani, Ray C ni mmoja wa mastaa ambao walikubali kuingiza nguvu zote kwenye mapambano hayo… Unajua kasidia watu wangapi mpaka sasa?
255 ilimpata Ray C ambae amesema mpaka sasa amesaidia vijana zaidi ya 70 kuachana na dawa za kulevya, kwa sasa wanaendelea kutibiwa na wanaendelea na shughuli nyingine kama kawaida.
CC
Ray C
Ray C anajitolea au inamlipa? Ukweli ni kwamba Ray C hapokei chochote, anachokifanya kwa sasa ni kusaidia watu walioathirika kama njia ya kusema ahsante kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyemsaidia kwa kiasi kikubwa kuacha kutumia dawa za kulevya.
Black Rhino amesema Video yake ya ‘Black Chata’ ilimsaidia vitu vingi sana ikiwemo kuwa nominated mwaka 2009 kwenye Tuzo zaChannel O ambapo kwa nafasi hiyo pekeyake ilimpa nafasi ya kupata connection na watu wengi akiwemo Producer na DJ mkubwa kutoka Capetown, Afrika Kusini ambae wamerekodi wimbo na video iitaachiwa any time kuanzia sasa.
TUNDA
Tundaman
Tundaman ameamua kutengenzea ngoma za Qaswida… hii ilikuwa idea yake ya muda mrefu kwani anamini safari yake kwenye muziki itaishia katika kuimba nyimbo za dini… Tunda amesema huu ni mwanzo mzuri kwake, album na video za Qaswida vikikamilika atasogeza mzigo mtaani kushare na watu wake !!
Ninayo 255 hapa, ukiplay utazikiliza story za mastaa wote leo June 26 2015.